Thursday, August 6, 2020

MKUTANO MKUU 2019

 Kikundi cha IKICHA huwa kina utamaduni wa kufanya mkutano mkuu na wanakikundi katika kila mwisho wa mwaka. Mkutanao huwa unapangwa na kikao cha mwezi wa 12 na shughuli za mkutano mkuu ni kujadili taarifa za kamati mbalimbali kama vile fedha na mikopo, uchumi na mipango, maafa na sherehe, katiba na sheria.

Taarifa hizi huwasilishwa na wenyeviti wa kamati hizo na kujadiliwa na wanakikundi. Lakini pia wajumbe wa mkutano mkuu wa mwaka huwa wanafanya uchaguzi kwa viongozi wa chama na makabidhiano huwa yanafanyika kwa viongozi wapya waliochaguliwa.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama wakifuatilia taarifa zilizokuwa zinawasilishwa.
Mkutano Mkuu ukiendelea huku wajumbe wakiendelea kupata viburudisho.
Mwenyekiti na Katibu Mkuu waliomaliza muda wao katika uongozi wakiwa wanaendesha mkutano mkuu.
Mwenyekiti aliyechaguliwa kwenye Mkutano Mkuu  Alex Kamalinge akitoa neno la shukrani baada ya kuchaguliwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu na aliyekaa hapo ni Katibu Mkuu wake Scola Wilson.
Baada ya uchaguzi makabidhiano huwa yanafanyika na hapo katika picha ni Ndg. Filbert Lukondo (kushoto) akiwa anamkabidhi majalada kwa mwenyekiti mpya wa kamati ya katiba na sheria Ndg. Emmanuel Msabaha.
Katibu Mkuu aliyechaguliwa Bi. Scola Wilson (kulia) akibadhiwa begi la mafaili na aliyekuwa Katibu Mkuu Ndg. Makoko Obadia.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wakifuatilia jambo.

Picha ya pamoja ya wanakikundi wa  IKICHA 

KANUNI ZA KIKUNDI CHA IKICHA


 

 KANUNI ZA IKICHA





S.L.P 44

KIGOMA.


E-MAIL: ikichagroup@gmail.com


TOLEO NA. 2, 2019







YALIYOMO                                                                                                                        UKURASA


SEHEMU YA KWANZA: UTANGULIZI

KAULI MBIU……………….…………………………………………………….………….……….3

NEMBO YA KIKUNDI……….…………………………………...………………...….................….3

ANUANI…………………………..…………………………………..…………….…..……………3

SEHEMU YA PILI: UANACHAMA

SIFA ZA MWANACHAMA………………………………………………………………………...3

HAKI ZA MWANACHAMA……………………………………………….………………………3

WAJIBU WA MWANACHAMA……………………………………………………………………4

SEHEMU YA TATU: UONGOZI WA KIKUNDI

UONGOZI WA KIKUNDI………………………..…………………………………................…..4

UCHAGUZI WA VIONGOZI…………………………………………………………...................4

SEHEMU YA NNE: MIKUTANO NA VIKAO VYA KIKUNDI

MIKUTANO NA VIKAO VYA KIKUNDI………………………………………………………..5

UDHURU…………………………………………………………………….…………..……….5

MSIBA………..…………………………………………………………………………………5

MAGONJWA…………………………………………………………………………………....5

KIKAZI…………………………………………………………….……………………………5

SAFARI YA LIKIZO………………………………………………………….............................5

SEHEMU YA TANO: MAPATO YA KIKUNDI

VYANZO VYA MAPATO YA KIKUNDI…..………..……………………………….…….…6

ADA YA KIINGILIO…………………………………………………………………………6

ADA YA MWEZI………………………………………………………………………………6

MICHANGO MINGINE…………………………………………………….....………………..7

MISIBA…………………………………………………………………………………………7

HARUSI…………………………………………………………………………………………7

MAGONJWA……………………………………………………..……………………………..8

ANAYEHAMA NJE YA MANISPAA…………………………………………………………8

MIKOPO………………………………………………………………………………………..8

MADENI YA KIKUNDI………………………………………………………………………10

SEHEMU YA SITA: UTUNZAJI WA MALI NA FEDHA ZA KIKUNDI

UTUNZAJI WA FEDHA ZA KIKUNDI…………………………………..……......…………..10

KIKOKOTOO CHA HISA…………………………………………………………………………10

SEHEMU YA SABA: KUVUNJIKA KWA KIKUNDI

KUVUNJIKA KWA KIKUNDI……………………………………………………………………11












SEHEMU YA KWANZA


1. 0 UTANGULIZI

1. 1 KAULI MBIU

1. 1.1 Kauli mbiu itatumika kwenye vikao,mikutano na matukio mbalimbali ya

kikundi kama salamu rasmi.

1.1.2 Kauli mbiu itatumika kwenye nyaraka zote zinazohusiana na kikundi.

I.2 NEMBO YA KIKUNDI

I.2.1 Nembo itatumika kwenye nyaraka zote zinazohusiana na kikundi.

I.2.2 Nembo itatumika kwenye sare zote za kikundi.

I.3 ANUANI

I.3.1 Itatumika kwenye barua zote za kikundi.


SEHEMU YA PILI


2.0 UANACHAMA

2.1 SIFA ZA MWANACHAMA

2. 1.1 Mtu yeyote anayeomba kujiunga na kikundi atapaswa kuwa na mdhamini

ndani ya kikundi atakayemsainia kwenye fomu ya kujiunga.

2.1.2 Mtu yeyote anayeomba kujiunga na kikundi atajadiliwa kwanza na

wanakikundi kabla ya kusajiliwa.

2.1.3 Kiambatisho kwenye fomu ya kujiunga na kikundi kitakuwa ni kivuli cha

Kitambulisho cha Taifa(NIDA)/Hati ya Kusafiria , kama nyaraka hizo hazipo

kiambatisho kitakuwa kitambulisho cha mpiga kura ama Leseni ya udereva.

2.1.4 Kila mwanachama atatakiwa kujaza fomu ya kujiunga na kikundi.

2.2 HAKI ZA MWANAKIKUNDI

2.2.1 Mwanakikundi akitaka kujitoa anatakiwa kutoa taarifa mwezi mmoja kabla kwa

maandishi ili aandaliwe stahiki zake.

2.2.2 Mwanakikundi anapaswa kulipa madeni yake yote anayodaiwa na kikundi

kabla ya kujitoa,kama atashindwa kulipa atakatwa kwenye Hisa/Stahiki

zake.


2.2.3 Uhuru wa kutoa maoni uwe na mipaka na maoni yaendane na dhima ya


kikundi.


2.2.4 Mwanakikundi atakuwa na uhuru wa kukopa fedha wakati wowote ikiwa


atatimiza vigezo na masharti ya ukopaji.


2.2.5 Mwanakikundi atabaki na uanachama wake ndani ya kikundi hata

akihama nje ya manispaa kwa kuzingatia sharti la kutokopa zaidi ya hisa

zake.


2.3 WAJIBU WA MWANAKIKUNDI


2.3.1 Kutoshiriki kwenye shughuli za kikundi kama vile magonjwa, misiba,

harusi, miradi n.k, faini yake itakuwa Tsh.5000/=kwa kila shughuli/tukio

ambalo mtu hakushiriki.


2.3.2 Mwanakikundi atakayekiuka maagizo rasmi ya kikundi atatozwa faini ya


Tsh. 5000/=.


2.3.3 Mwanachama atapewa maagizo rasmi ya kikundi mara mbili tu na

asipotekeleza kwa wakati aliopewa atatozwa faini ya Tsh.5000/=.

2.3.4 Mwanakikundi atatakiwa kutoa rambirambi kutokana na Vifo

vinavyotambuliwa na kikundi ambavyo ni mwanakikundi

kufariki,baba,mama,mme,mke au mtoto.


2.3.5 Vikao vya kikundi vitafanyika kila Jumapili ya kwanza ya kila mwezi.

2.3.6 Mwanakikundi ambaye hatatoa ushirirkiano wa kutosha /ipasavyo atapewa


adhabu mojawapo kati ya hizi zifuatazo;


a/ Onyo la mdomo.

b/ Faini ya Tsh.5,000/=.

2.3.7 Kikundi kitakuwa kinagharimia nauli zitakazokuwa zinatumika katika


shughuli za kikundi.


SEHEMU YA TATU


3.0 UONGOZI WA KIKUNDI

3.1 Kiongozi atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake atapewa adhabu

mojawapo kati ya hizi kulingana na kosa alilofanya, adhabu hizo ni;

a. Onyo la mdomo ama la maandishi.

b. Kulipa faini ya Tsh.10,000/=.

c. Fidia

d. Kusimamishwa uongozi kwa muda wa siku tisini (90).

e. Kuondolewa kwenye Uongozi.

3.2 Iwapo kiongozi atajiuzuru, atajitoa ama kutolewa kwenye kikundi ama

akihama uchaguzi wa nafasi yake utafanyika ndani ya mwezi mmoja.

3.3 Iwapo kiongozi atakuwa katika hali ya kuugua kwa muda wa miezi sita (06)

mfululizo nafasi yake itakaimiwa na mwanakikundi atakayependekezwa na

wanakikundi.

3.4 Iwapo kiongozi atafungwa jela nafasi yake itakaimiwa na mwanakikundi

atakayekuwa amependekezwa na wanakikundi hadi uchaguzi utakapofanyika.


3.5 UCHAGUZI WA VIONGOZI

I. Kwa nafasi ya Mwenyekiti na Katibu, yatapendekezwa majina matatu (3)

na kuyapigia kura za siri na mshindi wa kwanza ndiye atakayekuwa

MKUU na anayefuata kwa kura atakuwa MSAIDIZI wake.

II. Kwa nafasi ya Mhasibu, yatapendekezwa majina mawili na kuyapigia kura

za siri atakayepata kura nyingi ndiye atakayekuwa Mhasibu wa kikundi.


SEHEMU YA NNE

4.0 MIKUTANO NA VIKAO VYA KIKUNDI

4.1 UDHURU

a) MSIBA

i. Ruhusa za msiba zitatolewa iwapo mwanakikundi amefiwa na baba,

mama, mke, mume au mtoto.

b) MAGONJWA

i. Ruhusa za magonjwa zitatolewa iwapo mwanakikundi mwenyewe

amelazwa siku ya kikao.


c) KIKAZI

d) SAFARI YA LIKIZO

4.2 Mwanakikundi anawajibika kuwahi vikao na mikutano ya kikundi.

4.3 Mwanakikundi atatakiwa kutoa taarifa ya kuchelewa ama kutofika kwenye

vikao/mikutano ya kikundi saa moja kabla ya kikao/mkutano kuanza.

4.4 Iwapo mwanakikundi atachelewa kutoa taarifa ya kuchelewa kufika kwenye

kikao/mkutano atatozwa faini ya Tsh.1000/=.

4.5 Iwapo mwanakikundi hatatoa taarifa ya kuchelewa kufika kwenye

kikao/mkutano na akachelewa kufika kwenye kikao/mkutano atatozwa faini

ya Tsh.2000/=.

4.6 Iwapo mwanakikundi atachelewa kutoa taarifa ya kutohudhuria kwenye

kikao/mkutano atatozwa faini ya Tsh.3000/=.

4.7 Iwapo mwanakikundi hatatoa taarifa ya kutohudhuria kwenye kikao/mkutano

atatozwa faini ya Tsh.5000/=.

4.8 Iwapo mwanakikundi hatahudhuria kikao/mkutano kwa sababu zisizokubalika

katika Kanuni za Kikundi atatozwa faini ya Tsh.5000/=.

4.9 Iwapo mwanakikundi hatohudhuria kwenye kikao/mkutano atatozwa faini ya

Tsh.5000/=.

4.10 Hata kama kikao/mkutano utaahirishwa kwa sababu ya Akidi kutotimia, faini

iliyotajwa kwenye kifungu cha 4.3,4.4,4.5,4.6,4.7 na 4.8 itabaki pale pale.

4.11 Taarifa zote za kuchelewa ama kutohudhuria kikao/mkutano zitolewe kwa

Mwenyekiti/Katibu wa kikundi kwa njia ya meseji za simu/barua/kufika

mwenyewe kwenye kikao/mkutano.


SEHEMU YA TANO


5.0 MAPATO YA KIKUNDI

5.1 VYANZO VYA MAPATO YA KIKUNDI

5.1.1 ADA YA KIINGILIO

I. Mwanakikundi atasajiliwa kwenye kikundi baada ya kulipa kiingilio cha

Tsh. 50,000/=.

II. Kiingilio kitalipwa mara moja tu wakati wa kujiunga.


5.1.2 ADA YA MWEZI

I. Ada itakuwa inalipwa kila mwezi.

II. Ada ya mwezi ni Tsh. 12,000/=.

III. Kipindi cha Neema (Grace Period) cha kulipa ada kitaanza tarehe 01 hadi

tarehe 07 ya kila mwezi.

IV. Mwanakikundi atakayechelewa kulipa ada ya kila mwezi atapewa kipindi

cha Neema cha siku saba baada ya hapo kama atakuwa hajalipa

atatozwa faini ya Tsh.2000/= ambayo itakuwa ikiongezeka kwa kiasi

hicho hicho kila baada ya siku saba hadi hapo ada itakapokuwa

imetolewa.

V. Risiti itawasilishwa kwenye kikao cha kila mwezi.

VI. Mwanakikundi asipotoa Ada ya kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu (03)

mfululizo bila taarifa rasmi kwa uongozi atakuwa amejifuta uanachama wa

kikundi.

VII. Mwanakikundi atakayelipa ada kwa njia ya simu atalipa makato ya benki.

VIII. Mwanakikundi atahesabika amelipa ada baada ya kuwasilisha risiti ya

malipo.

IX. Mwanakikundi anatakiwa kulipa faini ndani ya miezi mitatu, na ikiingia

mwezi wa nne na kuendelea faini itaongezeka kwa asilimia mia(100%)

kwa kila mwezi.


5.1.3 MICHANGO MINGINE YA KIKUNDI

I. MISIBA

a) Kila mwanakikundi anatakiwa kutoa mchango wa Tsh.5000/= kwa ajili ya

pole kwa mfiwa.

b) Mchango huu utatolewa iwapo mwanachama ataondokewa na baba,

mama, mme, mke au mtoto.

c) Iwapo mwanakikundi amefariki kila mwanachama atatakiwa kutoa

mchango wa Tsh.10,000/=.

d) Mwanakikundi akifariki stahili zake zote atapewa mrithi aliyeainishwa

kwenye fomu ya kujiunga na uanachama.

e) Mwanakikundi ambaye hatakuwa ametoa mchango huu atakatwa

Tsh.5000/= au 10,000/= kutoka kwenye Ada yake ya kila mwezi.

f) Kiasi hicho kilichokatwa kwenye ada yake ya kila mwezi kitatakiwa

kirudishwe ndani ya mwezi mmoja tangu kilipokatwa.

g) Mchango wa rambirambi utatolewa ndani ya siku saba (7) tangu taarifa

ilipotolewa.

h) Mrithi atapewa stahili zake ndani ya siku 14 tangu ilipotolewa taarifa ya

msiba.


II. HARUSI

a) Mchango wa harusi utamhusu mwanakikundi tu.

b) Kila mwanakikundi atatoa Tsh.5000/= ambao utakuwa mchango kwa ajili

ya zawadi .

c) Mwanakikundi ambaye hatakuwa ametoa mchango huu atakatwa

Tsh.5000/= kutoka kwenye Ada yake ya kila mwezi.

d) Kiasi hicho kilichokatwa kwenye ada yake ya kila mwezi kitatakiwa

kirudishwe ndani ya mwezi mmoja tangu kilipokatwa.

e) Taarifa itolewe mwezi mmoja kabla ya harusi.


III. MAGONJWA

a) Kila mwanakikundi atatoa Tsh.5000/= kwa ajili ya mgonjwa.

b) Mwanakikundi ambaye hatakuwa ametoa mchango huu atakatwa Tsh.5000/=

kutoka kwenye Ada yake ya kila mwezi.

c) Kiasi hicho kilichokatwa kwenye ada yake ya kila mwezi kitatakiwa kirudishwe

ndani ya mwezi mmoja tangu kilipokatwa.

d) Mchango utatolewa kwa mwanachama ambaye amelazwa kuanzia siku tatu au

yuko kwenye hali mbaya sana.

e) Mwanakikundi atakayeumwa atapaswa kuleta vielelezo vya matibabu yake ili

achangiwe.

IV. ANAYEHAMA NJE YA MANISPAA

a. Kila mwanakikundi atatoa Tsh.5000/= kwa ajili ya zawadi ya kumuaga

Mwanakikundi anayehama.

b. Mwanakikundi ambaye hatakuwa ametoa mchango huu atakatwa

Tsh.5000/= kutoka kwenye Ada yake ya kila mwezi.

c. Kiasi hicho kilichokatwa kwenye ada yake ya kila mwezi kitatakiwa

kirudishwe ndani ya mwezi mmoja tangu kilipokatwa.

5.2 MIKOPO

5.2.1 Mwanakikundi anayeomba mkopo anatakiwa ajaze fomu ya maombi ya

mkopo.

5.2.2 Mwanakikundi anayetaka kukopa atatakiwa awe na mdhamini mmoja

ndani ya kikundi.

5.2.3 Mwanakikundi atapewa mkopo baada ya kutimiza masharti yote na iwapo

fedha ipo.

5.2.4 Utoaji wa mkopo utazingatia ombi lililotangulia.

5.2.5 Mwanakikundi atatakiwa kurejesha mkopo kwanza kabla ya kukopa tena.

5.2.6 Mwanakikundi mwenye deni lolote la ada,rejesho,faini ama michango

mingine hataruhusiwa kuchukua mkopo.

5.2.7 Mwanakikundi mpya ataruhusiwa kukopa baada ya miezi mitatu tangu

alipojiunga.

5.2.8 Mwanakikundi asiye na ajira ya kudumu ataruhusiwa kukopa kiasi

kinacholingana na hisa yake na kujumlisha kiasi cha nusu ya hisa yake.

5.2.9 Mwanakikundi atakayechukua mkopo atatakiwa kurejesha riba ya 10% ya

mkopo aliochukua.

5.2.10 Iwapo mwanakikundi atafariki akiwa na deni la kikundi na hisa zake ni

ndogo kuliko deni, atasamehewa deni hilo ila hisa zake zitabaki kuwa mali

ya kikundi.

5.2.11 Iwapo mwanakikundi atafariki akiwa na deni la kikundi na hisa zake ni

kubwa kuliko deni, hisa zake zitalipa deni hilo na kitakachobaki atapewa

mrithi wake.

5.2.12 Mwanakikundi atatakiwa kurejesha mkopo kama ifuatavyo;

I. 0000 - 100,000/=Marejesho ya Mkopo na Riba yafanyike ndani ya

mwezi mmoja (01).

II. 100,001-500,000/=Marejesho ya Mkopo na Riba yafanyike ndani ya

miezi mitatu (03).

III. 500,001- 1000,000/= Marejesho ya Mkopo na Riba yafanyike kila

mwezi ndani ya miezi sita (06) kwa uwiano wa moja ya sita (1/6).

IV. 1000,001- 1200,000/= Marejesho ya Mkopo na Riba yafanyike kila

mwezi ndani ya miezi saba (07) kwa uwiano wa moja ya saba(1/7).

V. 1200,001-1500,000/= Marejesho ya Mkopo na Riba yafanyike kila

mwezi ndani ya miezi nane (08) kwa uwiano wa moja ya nane(1/8).

5.2.13 Kama mwanakikundi atachelewa kurejesha rejesho lake la kila mwezi

atapewa kipindi cha Neema cha siku saba ,akiingia siku ya nane na

kuendelea rejesho lake litapigiwa 10% kama faini.

5.2.14 Iwapo mwanakikundi ameshindwa kurejesha mkopo wake kwa wakati na

kwa masharti aliyopewa sheria za kikundi na za nchi zitafuatwa

5.2.15 Mtu yeyote asiyekuwa mwanachama hataruhusiwa kupewa mkopo.

5.2.16 Mhasibu atatakiwa kuitaarifu Kamati ya Fedha na Mikopo kabla ya

kupitisha fomu ya mkopo wa mwanakikundi.

5.2.17 Watia saini watapewa nauli na kikundi watakapokuwa wanashughulikia

masuala ya fedha benki.


5.3 MADENI YA KIKUNDI.


I. Kila mwanakikundi anahusika kikamilifu na madeni ya kikundi kama

deni hilo halikusababishwa na uzembe wa mwanakikundi.

II. Deni binafsi la mwanakikundi si deni la kikundi na kikundi hakitahusika

kwa vyovyote vile.

III. Mkopo utakaohusu kikundi, wanakikundi wote washirikishwe katika

hatua zote na muhtasari uwepo wa kuthibitisha maazimio ya uchukuaji

wa mkopo huo.



SEHEMU YA SITA


6.0 UTUNZAJI WA MALI NA FEDHA ZA KIKUNDI

6.1 UTUNZAJI WA FEDHA ZA KIKUNDI.

I. Kila mwanakikundi ataweka Ada, Marejesho na Faini yake kwenye

Akaunti ya kikundi.

II. Mabadiliko yoyote ya Akaunti ya Benki ya kikundi yatatakiwa

kuwasilishwa, kujadiliwa na kupitishwa katika vikao vya kikundi.

III. Mhasibu na Kamati ya Fedha na Mikopo wataandaa Taarifa ya Fedha

ya Nusu mwaka na ya mwaka na kuiwasilisha kwa kamati Tendaji ya

kikundi.


6.2 KIKOKOTOO CHA HISA, kitakuwa;

JUMLA YA ADA ALIZOLIPA MWANACHAMA TANGU ALIPOJIUNGA NA

KIKUNDI JUMLISHA JUMLA YA FAIDA ILIYOPATIKANA KILA MWEZI KWA

MIEZI YOTE TANGU ALIPOJIUNGA NA KIKUNDI HADI TAREHE YA KUJITOA

/KUTOLEWA KWENYE KIKUNDI GAWANYA KWA IDADI YA WANACHAMA

KWA KILA MWEZI.

SAWA NA;


JUMLA YA ADA + JUMLAYA FAIDA YA KILA MWEZI KWA MIEZI YOTE


IDADI YA WANACHAMA KILA MWEZI


SEHEMU YA SABA


7 .0 KUVUNJIKA KWA KIKUNDI

I. Kikundi kitavunjika iwapo robo tatu ya wanakikundi wameridhia kuvujika.

II. Endapo kikundi kitabaki na wanakikundi wawili, kitatakiwa kivunjwe.

III. Kikundi kikivujwa/kuvunjika wanakikundi ambao watakuwa hai ndio watakao

gawana mali zote za kikundi.

IV. Maamuzi ya kuvunja kikundi yatafanyika katika kikao halali cha kikundi na

muhtasari utaandikwa.

V. Kabla ya kuvunja kikundi, pesa zote za kikundi zitatakiwa kuwekwa kwenye

Akaunti ya kikundi.

VI. Kabla ya kuvunja kikundi, madeni yote ya kikundi yanatakiwa kulipwa kwanza.

VII. Kabla ya kuvunja kikundi, mali zote za kikundi zitatakiwa kuwasilishwa

kwenye kikao cha kuvunja kikundi.


IKICHA…,


TUINUANE KATIKA MAENDELEO

KATIBA YA KIKUNDI CHA INUA KIPATO CHAKO (IKICHA)

(IKICHA)







S.L.P 44
KIGOMA.

E-MAIL: ikichagroup@gmail.com

KATIBA
TOLEO NA. 2, 2019















YALIYOMO                                                                UKURASA

SEHEMU YA KWANZA: UTANGULIZI
Jina la Kikundi………………………………………………………………………………………….4
Kauli Mbiu ya Kikundi………………………………………………………………………………….4
Nembo ya Kikundi…………………………………………...………………………………………….4
Anuani ya Kikundi……………………………………………………...……………………………….4

SEHEMU YA PILI: MALENGO YA KIKUNDI
Misingi ya Kikundi (Group Core Values)……………………………………………………………….5
Lengo Kuu la Kikundi…………………………………………………………………………………..5
Malengo Mahususi ya Kikundi………………………………………………………………………….5

SEHEMU YA TATU: IDADI YA WANACHAMA,JINSIA NA LUGHA
Idadi ya Wanachama……………………………………………………………………………………5
Jinsia…………………………………………………………………………………………………….5
Lugha……………………………………………………………………………………………………5

SEHEMU YA NNE: UANACHAMA
Kujiunga na Kikundi…………………………………………………………………………………….6
Sifa za Mwanachama…………………………………………………………………..………………..6
Haki za Mwanachama…………………………………………………………………….…………….6
Wajibu wa Mwanachama………………………………………………………………...…………..…6
Ukomo wa Mwanachama……………………………………………………………...……………..…6

SEHEMU YA TANO: UONGOZI WA KIKUNDI
Muundo wa Uongozi……………………………………………………………………………………7
Majukumu ya Viongozi……………………………………..…………………………………………..8
Mwenyekiti…………………………………………………...…………………………………………8
Majukumu ya Mwenyekiti ………….…………………………………………………………….......8
Mwenyekiti Msaidizi…………………………………………………………………………………….8
Majukumu ya Mwenyekiti Msaidizi………………………………………………………………….......8
Katibu…………………………………………………………………………………………………….8
Majukumu ya Katibu…………………………………………………………………………………....8
Katibu Msaidizi…………………………………………………………………………………………..8
Majukumu ya Katibu Msaidizi…………………………………………………………………………...8
Mhasibu………………………………………………………………………………………………....8
Majukumu ya Mhasibu………………………………………………………………………………..9
Kamati za Kikundi……………………………………………………………………………………...9
Kamati ya Katiba na Sheria………………………………………………………………………..….9
Wajumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria……………………………………………………………....9
Majukumu ya Kamati……………………………………………………………………………………9
Kamati ya Fedha na Mikopo………………………………………………………………………….….9
Wajumbe wa Kamati ya Fedha na Mikopo……………………………………………………………..9
Majukumu ya Kamati………………………………………………………..……………………….…9
Kamati ya Maafa na Sherehe………………………………………………………………………….….9
Wajumbe wa Kamati ya Maafa na Sherehe…………………………………………………………..…..9
Majukumu ya Kamati……………………………………………………………………………….…10
Kamati ya Uchumi na Mipango……………………………………………………………………….10

KATIBA YA IKICHA
Wajumbe wa Kamati ya Uchumi na Mipango…………………………………………………….......10
Majukumu ya Kamati………………………………………………………………………………....10
Muda wa Uongozi………………………………………………………………………………………10

SEHEMU YA SITA: MIKUTANO NA VIKAO VYA KIKUNDI
Mkutano Mkuu………………………………………………………………………………………..10
Majukumu ya Mkutano Mkuu………………………………………………………………………...10
Vikao vya Kikundi………………………………………………………………………………………11
Majukumu ya Vikao…………………………………………………………………………………...11
Vikao vya dharura………………………………………………………………………………………11
Kamati Tendaji…………………………………………………………………………………………..11
Vikao vya Kamati Tendaji………………………………………………………………………………11
Majukumu ya Kamati Tendaji…………………………………………………………………………11

SEHEMU YA SABA: MAPATO YA KIKUNDI
Vyanzo vya Mapato ya Kikundi……………………………………………………………………….12
Ada ya Kiingilio……………………………………………………………………………………….12
Ada ya kila mwezi……………………………………………………………………………………12
Faida kutokana na Miradi…………………………………………………………………………...12
Riba ya Mikopo……………………………………………………………………………………….12
Miradi mbalimbali…………………………………………………………………………………...12
Faini mbalimbali………………………………………………................…………………………...12
Michango Mingine …………………………………………….............................................………..12
Harusi……………………………………………………………………………………………….12
Magonjwa.………………………………………………………… ……………………………..12
Misiba……………………………………………………………………………..………………….12
Anayehama Nje ya Manispaa…………………………………………………………………………12
Mikopo…………………………………………………………………………………………..……12
Madeni ya Kikundi………………………………………………..……………………………………12

SEHEMU YA NANE: UTUNZAJI WA MALI NA FEDHA ZA KIKUNDI
Utunzaji wa Mali na Fedha za Kikundi……………………………………………………………….13
Upotevu na Uharibifu wa Mali ya Kikundi…………………………………………………..………13

SEHEMU YA TISA: MAREKEBISHO YA KATIBA NA KUVUNJIKA KWA KIKUNDI
Marekebisho ya Katiba ya Kikundi…………………………………………………………….……….13
Kuvunjika Kwa Kikundi……………………………………………………………………………….13

SEHEMU YA KUMI: ORODHA YA WANACHAMA NA SAHIHI ZAO
Orodha ya Wanachama na Sahihi za Wanachama…………………………………………….……..14












SEHEMU YA KWANZA

1.0 UTANGULIZI


1. 1 JINA LA KIKUNDI

IKICHA (INUA KIPATO CHAKO) ni umoja wa baadhi ya Watu wanaoishi
katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji waliokubaliana kuanzisha kikundi kwa malengo
mbalimbali na lengo kuu likiwa Kuwezesha mwanakikundi kujikwamua kiuchumi kwa njia
ya kuweka na kukopa.Kikundi hiki kilianzishwa rasmi tarehe 13/12/2015 kikiwa na
idadi ya wanachama kumi na moja (11).
Katiba hii itajulikana kama Katiba ya kikundi cha IKICHA ya mwaka 2019 ambayo
imetokana na mabadiliko ya katiba, Toleo Na.1,2015 na itakuwa ndio muongozo wa
kuendesha shughuli zote za kikundi.

1.2 KAULI MBIU YA KIKUNDI

1.2.1 Kauli mbiu ya kikundi ni “TUINUANE KATIKA MAENDELEO”

1.3 NEMBO YA KIKUNDI

1.3.1 .Kikundi kitakuwa na NEMBO
1.3.2 NEMBO ya kikundi itakuwa na alama zifuatazo:-
I. Ramani ya Afrika
II. Pesa
III. Nyumba
IV. Gari
V. Mti
VI. Ngazi
VII. Mtu akipanda ngazi


1.4. ANUANI
KIKUNDI CHA INUA KIPATO CHAKO (IKICHA),
MTAA WA LAKE TANGANYIKA.
S.L.P 44,
KIGOMA.
E-mail: ikichagroup@gmail.com


1.5 MISINGI YA KIKUNDI (GROUP CORE VALUES)

I. Upendo
II. Uadilifu
III. Uaminifu
IV. Ukweli na Uwazi
V. Kuheshimiana
VI. Uwajibikaji

KATIBA YA IKICHA

VII. Umoja na Ushirikiano
VIII. Usiri
IX. Bidii
X. Maendeleo

SEHEMU YA PILI

2.0 MALENGO YA KIKUNDI

2.1 LENGO KUU LA KIKUNDI
2.1.1 Kuwezesha mwanakikundi kujikwamua kiuchumi.

2.2 MALENGO MAHUSUSI YA KIKUNDI
I. Kuweka na Kukopa.
II. Kusaidiana katika Shida na Raha.
III. Kuelimishana katika masuala ya Kiuchumi.
IV. Kuanzisha Miradi mbalimbali ya Kiuchumi.

SEHEMU YA TATU

3.0 IDADI YA WANACHAMA,JINSIA NA LUGHA

3.1. IDADI YA WANACHAMA
3.1.1 Kikundi kitakuwa na wanachama 30 tu.
3.2. JINSIA.
3.2.1 Kikundi kitakuwa cha Jinsia zote.
3.3 LUGHA
3.3.1 Lugha ya mawasiliano itakuwa Kiswahili.

SEHEMU YA NNE

4.0 UANACHAMA

4.1 KUJIUNGA NA KIKUNDI
4.1.1 Ni muda wowote kama kuna nafasi.

IV.2 SIFA ZA MWANACHAMA.
I.Awe na umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea.
II.Awe ameajiriwa au kujiajiri.
III.Awe mwaminifu na mwenye tabia njema.
IV.Awe mkazi katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
V.Awe mtiifu kwa katiba,sheria na kanuni za kikundi.


4.3 HAKI ZA MWANACHAMA
I.Ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika uongozi wa kikundi.
II.Ana uhuru wa kutoa maoni.
III. Ana haki ya kujitoa uanakikundi.
IV.Ana haki ya kusaidiwa katika shida na raha.
V.Ana haki ya kujua mapato na Matumizi ya kikundi.
VI.Ana haki ya kujua michango yake.
VII.Ana haki ya kukopa fedha kwenye kikundi.

4.4 WAJIBU WA MWANACHAMA
I.Kuhudhuria vikao/mikutano ya kikundi.
II.Kuchangia michango ya kikundi.
III.Kushiriki shughuli zote za kikundi
IV.Kutunza siri za kikundi.
V.Kulipa mali ya kikundi akiharibu au kupoteza kwa uzembe au makusudi.
VI.Kuwapenda na kuwajali wanakikundi wenzake.
VII.Kulinda na kutunza mali za kikundi.
VIII. Kutoa ushauri kuhusu maendeleo ya kikundi.
IX. Kutekeleza maagizo rasmi ya Kikundi.

4.5 UKOMO WA MWANACHAMA
I. Kifo
II.Kujitoa kwa hiari.
III.Kuvunjika kwa kikundi.
IV.Kufutwa/kusimamishwa na kikundi.
V.Kutohudhuria vikao vitatu mfululizo bila taarifa rasmi na kushindwa kulipa faini yake.
VI.Kutohudhuria kwenye matukio matatu mfululizo ya kikundi bila taarifa na kushidwa
kulipa faini ya kosa hilo.

SEHEMU YA TANO

5.0 UONGOZI WA KIKUNDI

5.1 MUUNDO WA UONGOZI

MWENYEKITI

KATIBA YA IKICHA

MWENYEKITI MSAIDIZI

KATIBU

KATIBU MSAIDIZI

MHASIBU

KAMATI ZA KIKUNDI

WAJUMBE

5.2 MAJUKUMU YA VIONGOZI
5.2.1 MWENYEKITI
5.2.1.1 MAJUKUMU YA MWENYEKITI
I.Kuongoza vikao/ mikutano yote ya kikundi.
II.Kuwa msemaji mkuu wa kikundi.
III.Kusimamia katiba, sheria na kanuni za kikundi.
IV.Kukagua mapato na matumizi ya kikundi.
V. Kusimamia mali za kikundi.
VI. Kugawa kazi kwa wanakikundi.
VII. Kutunza mali za kikundi anazotumia kama mwenyekiti.

5.2.2 MWENYEKITI MSAIDIZI
5.2.2.1 Ni Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria.
5.2.2.2 MAJUKUMU YA MWENYEKITI MSAIDIZI
I.Atatekeleza majukumu ya Mwenyekiti wakati Mwenyekiti anapokuwa hayupo kwa
udhuru wowote ule.
II.Kumsaidia Mwenyekiti.


5.2.3 KATIBU

5.2.3.1 MAJUKUMU YA KATIBU
I.Mtendaji mkuu wa kikundi.
II.Kuitisha vikao vya kikundi.
III.Kuandika mihtasari ya vikao na mikutano ya kikundi.
IV.Kutunza kumbukumbu zote za kikatibu.

5.2.4 KATIBU MSAIDIZI

5.2.4.1 Ni mjumbe wa Kamati ya Fedha na Mikopo.

5.2.4.2 MAJUKUMU YA KATIBU MSAIDIZI
I.Atatekeleza majukumu ya Katibu wakati katibu anapokuwa hayupo kwa udhuru
wowote.
II.Kumsaidia Katibu.
III.Atakaimu nafasi ya Mhasibu endapo Mhasibu hatakuwepo.

5.2.5 MHASIBU
5.2.5.1 Mhasibu atatakiwa kuwa mwenye ajira ya kudumu.
5.2.5.2 Atakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mikopo.

5.2.5.3 MAJUKUMU YA MHASIBU

I.Kutunza kumbukumbu za fedha za kikundi .
II.Kuandaa na Kutoa taarifa ya Mapato na Matumizi ya nusu mwaka na ya
mwaka mzima.
III.Kuwakumbusha wanakikundi juu ya michango yao na madeni ya kila mwezi.
IV.Kufuatilia mikopo kwa wanachama waliochukua mikopo na kuhakikisha
inarejeshwa kwa wakati.
V. Kutunza vifaa vya kiuhasibu.
VI.Kuandaa vifaa na nyaraka za kiuhasibu.
VII.Ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mikopo.

5.3 KAMATI ZA KIKUNDI

5.3.1 KAMATI YA KATIBA NA SHERIA

5.3.1.1 WAJUMBE WA KAMATI YA KATIBA NA SHERIA

I. Mwenyekiti Msaidizi wa Kikundi (Mwenyekiti wa Kamati).
II. Wajumbe 2 wa kuchaguliwa na kikundi.
5.3.1.2 Mjumbe mmoja wa Kamati hii atakuwa mjumbe wa Kamati ya Fedha na Mikopo.

5.3.1.3 MAJUKUMU YA KAMATI
I.Kusimamia Katiba na Sheria za kikundi.
II.Kuandaa na kutoa fomu za kujiunga na kikundi.
III.Kupendekeza maboresho ya Katiba na Sheria.

5.3.2 KAMATI YA FEDHA NA MIKOPO

5.3.2.1 WAJUMBE WA KAMATI YA FEDHA NA MIKOPO
I. Mhasibu (Mwenyekiti wa Kamati)

KATIBA YA IKICHA
II. Katibu Msaidizi
III.Mjumbe mmoja kutoka Kamati ya Katiba na Sheria.

5.3.2.2 MAJUKUMU YA KAMATI
I.Kusimamia utoaji na urejeshaji wa mikopo.
II.Kuandaa na kutoa fomu za mikopo
III.Kuandaa na Kutoa Taarifa ya Mikopo.
IV.Kutafuta na kufuatilia wapi mikopo inapatikana.
V. Kuandaa na Kutoa taarifa ya Mapato na Matumizi ya nusu mwaka na ya
mwaka mzima.

5.3.3 KAMATI YA MAAFA NA SHEREHE

5.3.3.1 WAJUMBE WA KAMATI YA MAAFA NA SHEREHE

I.Kamati itakuwa na wajumbe watatu (03) wa kuchaguliwa na kikundi.

5.3.3.2 MAJUKUMU YA KAMATI
I. Kutoa Taarifa ya Maafa na Sherehe kwa wanachama.
II. Kupendekeza namna ya kutatua matatizo hayo.
III.Kusimamia michango ya Maafa na Sherehe.
IV. Kuandaa na Kusimamia sherehe za kikundi.

5.3.4 KAMATI YA UCHUMI NA MIPANGO

5.3.4.1 WAJUMBE WA KAMATI YA UCHUMI NA MIPANGO

I.Kamati itakuwa na wajumbe watatu (03) wa kuchaguliwa na kikundi.

5.3.4.2 MAJUKUMU YA KAMATI
I. Kubuni na kuanzisha miradi.
II. Kushauri kikundi masuala ya uchumi.
III.Kuratibu mafunzo ya ujasiriamali kwa kikundi.
IV.Kuandaa malengo ya mwaka.
V Kusimamia miradi ya kikundi.

5.4. MUDA WA UONGOZI
I.Uongozi utakuwa madarakani kwa muda wa mwaka mmoja (1) tu.
II.Kiongozi anaweza kuchaguliwa tena kuwa kiongozi baada ya muda wake wa
uongozi kukamilika.
III. Mwanachama hataweza kuchaguliwa na kuitumikia nafasi moja kwa muda wa
zaidi ya miaka mitatu (03) mfululizo.
IV.Kiongozi aliyetumikia nafasi moja kwa miaka mitatu mfululizo anaweza
kuchaguliwa kwenye nafasi nyingine.

SEHEMU YA SITA
6.0 MIKUTANO NA VIKAO VYA KIKUNDI
6.1 MKUTANO MKUU

KATIBA YA IKICHA
6.1.1 Mkutano mkuu wa kikundi utafanyika mara moja kwa kila mwaka.
6.1.2 Tarehe ya mkutano mkuu kufanyika itapangwa na kikao cha mwezi wa kumi na
mbili (12).

6.1.3 MAJUKUMU YA MKUTANO MKUU
I.Kupokea na kujadili taarifa ya fedha.
II. Kujadili jambo lilojitokeza kama vile kupokea wanachama wapya, kufukuza au
kutoa ushauri kwa wanachama kuhusu mwenendo mzima wa mwanachama.
III.Kujadili mwanachama anayetaka kujitoa.
IV.Kujadili maendeleo ya kikundi ya mwaka.
V.Kupokea na kujadili taarifa za kamati za kikundi.
VI.Kujadili na kupitisha miradi ya kikundi.
VII. Kufanya uchanguzi wa viongozi wa Kikundi.
VIII. Kupanga namna bora ya kuinua kikundi kiuchumi.

6.2 VIKAO VYA KIKUNDI
6.2.1 Kutakuwa na vikao kumi na mbili (12) kwa mwaka.
6.2.2 Vikao vyote kumi na mbili vitafanyika kila Jumapili ya kwanza ya kila mwezi.

6.2.3 MAJUKUMU YA VIKAO
I. Kupokea ADA ya kila mwezi.
II. Kupokea maombi ya mikopo.
III. Kujadili maendeleo ya kikundi.
IV. Kupokea marejesho ya mkopo.
V. Kupokea maombi ya wanachama wapya.
VI. Kujadili ukomo wa mwanachama.
VII. Kupokea mapendekezo ya mabadiliko ya katiba na kanuni.
VIII. Kupokea na kujadili taarifa mbalimbali za kikundi.

6.3 VIKAO VYA DHARURA
I.Kutakuwa na Vikao vya dharura kama ikibidi viwepo.

6.4. KAMATI TENDAJI
6.4.1 Itaundwa na Mwenyekiti,Mwenyekiti Msaidizi,Katibu,Katibu Masidizi na Mhasibu.

6.4.2 VIKAO VYA KAMATI TENDAJI
I Kamati Tendaji itakaa mara moja kwa mwezi kabla ya kila kikao.
II Kamati Tendaji itafanya kikao mwezi mmoja kabla ya Mkutano Mkuu.

6.4.3 MAJUKUMU YA KAMATI TENDAJI
I.Kuandaa agenda za mkutano mkuu.
II.Kuandaa taarifa ya fedha.
III.Kushughulikia masuala ya nidhamu.
IV.Kupitia na kujadili miradi ya kikundi.
V.Kusimamia maendeleo ya kikundi.

KATIBA YA IKICHA
VI.Kujadili maombi ya wanachama wapya.
VII.Kupokea,Kujadili na Kuwasilisha Mapendekezo ya Marekebisho ya Katiba
kwenye Kikao au Mkutano mkuu.
VIII.Kuandaa agenda za Vikao na Mkutano mkuu.
SEHEMU YA SABA

7.0 MAPATO YA KIKUNDI

7.1 VYANZO VYA MAPATO YA KIKUNDI

7.1.1 Ada ya kiingilio
I. Kila mwanachama anapaswa kulipa ada ya kiingilio.
II. Kiingilio ni mali ya kikundi.

7.1.2 Ada ya kila mwezi.
I. Kila mwanachama anapaswa kulipa Ada kila mwezi.

II. Ada ni mali ya mwanachama.
7.1.3 Faida kutokana na Miradi.
7.1.4. Riba ya Mikopo
7.1.5 Faini mbalimbali.
7.1.6 Miradi mbalimbali

7.1.7 MICHANGO MINGINE
I.HARUSI
a) Mwanachama akiwa na Harusi atachangiwa.
II.MAGONJWA
a) Mwanachama akilazwa kuanzia siku tatu mfululizo atachangiwa.
b) Mwanachama atakayepewa rufaa ya matibabu nje ya Wilaya ya Kigoma
atachangiwa .
III.MISIBA
a) Mwanachama akifariki kila mwanakikundi atatoa rambirambi.
b) Mwanachama akifiwa atapewa rambirambi kutoka kwa kila mwanachama.
IV.ANAYEHAMA NJE YA MANISPAA
a) Mwanachama atakayehama nje ya Manispaa atachangiwa.

7.2 MIKOPO
7.2.1 Kila mwanachama atakuwa na haki ya kukopa kwenye kikundi.
7.2.2 MADENI YA KIKUNDI
I.Kila mwanakikundi anahusika kikamilifu na madeni ya kikundi kama si kwa uzembe.
II.Deni binafsi la mwanakikundi si deni la kikundi na kikundi hakitahusika kwa
vyovyote vile.
III.Mkopo utakaohusu kikundi wanachama wote washirikishwe katika hatua zote za
kuchukua mkopo huo na muhtasari uwepo wa kuthibitisha uchukuaji wa mkopo huo.



SEHEMU YA NANE

8.0 UTUNZAJI WA MALI NA FEDHA ZA KIKUNDI
8.1.UTUNZAJI WA MALI NA FEDHA ZA KIKUNDI

I.Kikundi kitakuwa na akaunti benki ambamo fedha zote za kikundi zitatunzwa.
II.Waweka sahihi katika akaunti watakuwa ni :-
a) Mwenyekiti wa Kikundi.
b) Mhasibu wa Kikundi.
c) Katibu wa Kikundi.
d) Mwanachama mmoja ambaye si mjumbe wa Kamati Tendaji.
8.2.UPOTEVU NA UHARIBIFU WA MALI YA KIKUNDI
I. Iwapo itabainika mwanakikundi amepoteza au kuharibu mali ya kikundi itabidi
alipe au afidie upotevu huo au uharibifu huo .Endapo atashindwa kutekeleza agizo
alilopewa sheria na taratibu za kikundi na za nchi zitafuatwa.

SEHEMU YA TISA

9.0 MAREKEBISHO YA KATIBA NA KUVUNJIKA KWA KIKUNDI

9.1 MAREKEBISHO YA KATIBA YA KIKUNDI

I.Marekebisho ya Katiba yatafanyika endapo kutakuwa na uhitaji.
II.Marekebisho ya Katiba yatafanyika iwapo robo tatu ya wanachama wameridhia.
III.Mapendekezo ya Marekebisho ya Katiba yatawasilishwa kwenye kamati ya Katiba
na Sheria kwa maandishi.

9.2 KUVUNJIKA KWA KIKUNDI
I. Kikundi kitavunjika iwapo robo tatu ya wanachama wameridhia.
II.Kufutiwa usajili na Serikali.

SEHEMU YA KUMI


10.0 ORODHA YA WANACHAMA

NA      MAJINA KAMILI                         JINSIA                          WADHIFA                    
1 ELIAS LUZARIA                                     ME                                  MJUMBE                      
2 MAKOKO OBADIA                                ME                                   MJUMBE                      
3 KELVIN E. NGOWI                                 ME                                   MHASIBU                    
4 FILBERT S.LUKONDO                           ME                                    MJUMBE                    
5 KULWA MATHIAS                                   ME                                   MJUMBE                     
6 VITUS TONDELO                                     ME                                   MJUMBE                     
7 SCOLA WILSON                                        KE                                   KATIBU                    
8 EMMANUEL MSABAHA                         ME                                  MJUMBE                      
9 LEAH MOSES                                             KE                                 MJUMBE                     
10 ALEX KAMALINGE                                 ME                               MWENYEKITI                  
11 VERONICA MGOZI                                 KE                                 MJUMBE                   
12 ABDALLAH JUMA                                   ME                               MJUMBE 
13 NEEMA TITO                                            KE                                MJUMBE
14 ZUBERI MROGORO                              ME                                  MJUMBE
15 MARUZUKU SELEMANI                       ME                                MJUMBE
16 NICHOLOUS NDELE                             ME                                  MJUMBE
17 SAMWEL JOSEPH                                  ME                                  MJUMBE
18
19

HISTORIA YA KIKUNDI CHA INUA KIPATO CHAKO (IKICHA)

KIKUNDI CHA INUA KIPATO CHAKO


“TUINUANE KATIKA MAENDELEO’’

Kikundi cha Inua Kipato Chako (IKICHA) kilianzishwa mnamo tarehe 13/12/2015 kikiwa na
idadi ya wanachama kumi na moja (11) na sasa kina jumla ya wanachama kumi na tisa (19).
Kikundi hiki ni ni umoja wa baadhi ya Watu wanaoishi katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji
waliokubaliana kuanzisha kikundi kwa malengo mbalimbali na lengo kuu likiwa Kuwezesha
mwanakikundi/mwanachama kujikwamua kiuchumi kwa njia ya kuweka na kukopa.
Kikundi hiki kilikuwa chini ya uongozi wa Elias Luzaria kama Mwenyekiti, Proches Fabian
kama Mwenyekiti Msaidizi, Makoko Obadia kama Katibu, Vitus Tondelo kama Katibu Msaidizi
na Gabriel Ng’honoli kama Mhasibu. Hii ndio Kamati Tendaji ya kwanza katika kikundi hiki.
Kwa sasa kikundi hiki kinaongozwa na Alex Kamalinge kama Mwenyekiti, Emmanuel Msabaha kama Mwenyekiti Msaidizi, Scola Wilson kama Katibu, Kulwa Mathias kama Katibu Msaidizi
au Kaimu Mhasibu na Kelvin Ngowi kama Mhasibu wa kikundi.

ANUANI YA KIKUNDI:

KIKUNDI CHA INUA KIPATO CHAKO (IKICHA),
MTAA WA LAKE TANGANYIKA,
S.L.P 44,
KIGOMA.
E-mail: ikichagroup@gmail.com

IKICHA kimejengwa katika misingi ifuatayo:

I. Upendo
II. Uadilifu
III. Uaminifu
IV. Ukweli na Uwazi
V. Kuheshimiana
VI. Uwajibikaji
VII. Umoja na Ushirikiano
VIII. Usiri
IX. Bidii
X. Maendeleo

Kikundi cha IKICHA kimelenga kumwezesha mwanakikundi kujikwamua kiuchumi katika
yafuatayo:
I. Kuweka na Kukopa.
II. Kusaidiana katika Shida na Raha.
III. Kuelimishana katika masuala ya Kiuchumi.
IV. Kuanzisha Miradi mbalimbali ya Kiuchumi.

Kikundi hiki bado kinahitaji kupata wanachama wapya ila wawe na sifa zifuatazo:
I. Awe na umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea.
II. Awe ameajiriwa au kujiajiri.
III. Awe mwaminifu na mwenye tabia njema.
IV. Awe mkazi katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
V. Awe mtiifu kwa katiba,sheria na kanuni za kikundi.