Thursday, August 6, 2020

HISTORIA YA KIKUNDI CHA INUA KIPATO CHAKO (IKICHA)

KIKUNDI CHA INUA KIPATO CHAKO


“TUINUANE KATIKA MAENDELEO’’

Kikundi cha Inua Kipato Chako (IKICHA) kilianzishwa mnamo tarehe 13/12/2015 kikiwa na
idadi ya wanachama kumi na moja (11) na sasa kina jumla ya wanachama kumi na tisa (19).
Kikundi hiki ni ni umoja wa baadhi ya Watu wanaoishi katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji
waliokubaliana kuanzisha kikundi kwa malengo mbalimbali na lengo kuu likiwa Kuwezesha
mwanakikundi/mwanachama kujikwamua kiuchumi kwa njia ya kuweka na kukopa.
Kikundi hiki kilikuwa chini ya uongozi wa Elias Luzaria kama Mwenyekiti, Proches Fabian
kama Mwenyekiti Msaidizi, Makoko Obadia kama Katibu, Vitus Tondelo kama Katibu Msaidizi
na Gabriel Ng’honoli kama Mhasibu. Hii ndio Kamati Tendaji ya kwanza katika kikundi hiki.
Kwa sasa kikundi hiki kinaongozwa na Alex Kamalinge kama Mwenyekiti, Emmanuel Msabaha kama Mwenyekiti Msaidizi, Scola Wilson kama Katibu, Kulwa Mathias kama Katibu Msaidizi
au Kaimu Mhasibu na Kelvin Ngowi kama Mhasibu wa kikundi.

ANUANI YA KIKUNDI:

KIKUNDI CHA INUA KIPATO CHAKO (IKICHA),
MTAA WA LAKE TANGANYIKA,
S.L.P 44,
KIGOMA.
E-mail: ikichagroup@gmail.com

IKICHA kimejengwa katika misingi ifuatayo:

I. Upendo
II. Uadilifu
III. Uaminifu
IV. Ukweli na Uwazi
V. Kuheshimiana
VI. Uwajibikaji
VII. Umoja na Ushirikiano
VIII. Usiri
IX. Bidii
X. Maendeleo

Kikundi cha IKICHA kimelenga kumwezesha mwanakikundi kujikwamua kiuchumi katika
yafuatayo:
I. Kuweka na Kukopa.
II. Kusaidiana katika Shida na Raha.
III. Kuelimishana katika masuala ya Kiuchumi.
IV. Kuanzisha Miradi mbalimbali ya Kiuchumi.

Kikundi hiki bado kinahitaji kupata wanachama wapya ila wawe na sifa zifuatazo:
I. Awe na umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea.
II. Awe ameajiriwa au kujiajiri.
III. Awe mwaminifu na mwenye tabia njema.
IV. Awe mkazi katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
V. Awe mtiifu kwa katiba,sheria na kanuni za kikundi.

No comments:

Post a Comment