KANUNI ZA IKICHA
S.L.P 44
KIGOMA.
E-MAIL: ikichagroup@gmail.com
TOLEO NA. 2, 2019
YALIYOMO UKURASA
SEHEMU YA KWANZA: UTANGULIZI
KAULI MBIU……………….…………………………………………………….………….……….3
NEMBO YA KIKUNDI……….…………………………………...………………...….................….3
ANUANI…………………………..…………………………………..…………….…..……………3
SEHEMU YA PILI: UANACHAMA
SIFA ZA MWANACHAMA………………………………………………………………………...3
HAKI ZA MWANACHAMA……………………………………………….………………………3
WAJIBU WA MWANACHAMA……………………………………………………………………4
SEHEMU YA TATU: UONGOZI WA KIKUNDI
UONGOZI WA KIKUNDI………………………..…………………………………................…..4
UCHAGUZI WA VIONGOZI…………………………………………………………...................4
SEHEMU YA NNE: MIKUTANO NA VIKAO VYA KIKUNDI
MIKUTANO NA VIKAO VYA KIKUNDI………………………………………………………..5
UDHURU…………………………………………………………………….…………..……….5
MSIBA………..…………………………………………………………………………………5
MAGONJWA…………………………………………………………………………………....5
KIKAZI…………………………………………………………….……………………………5
SAFARI YA LIKIZO………………………………………………………….............................5
SEHEMU YA TANO: MAPATO YA KIKUNDI
VYANZO VYA MAPATO YA KIKUNDI…..………..……………………………….…….…6
ADA YA KIINGILIO…………………………………………………………………………6
ADA YA MWEZI………………………………………………………………………………6
MICHANGO MINGINE…………………………………………………….....………………..7
MISIBA…………………………………………………………………………………………7
HARUSI…………………………………………………………………………………………7
MAGONJWA……………………………………………………..……………………………..8
ANAYEHAMA NJE YA MANISPAA…………………………………………………………8
MIKOPO………………………………………………………………………………………..8
MADENI YA KIKUNDI………………………………………………………………………10
SEHEMU YA SITA: UTUNZAJI WA MALI NA FEDHA ZA KIKUNDI
UTUNZAJI WA FEDHA ZA KIKUNDI…………………………………..……......…………..10
KIKOKOTOO CHA HISA…………………………………………………………………………10
SEHEMU YA SABA: KUVUNJIKA KWA KIKUNDI
KUVUNJIKA KWA KIKUNDI……………………………………………………………………11
SEHEMU YA KWANZA
1. 0 UTANGULIZI
1. 1 KAULI MBIU
1. 1.1 Kauli mbiu itatumika kwenye vikao,mikutano na matukio mbalimbali ya
kikundi kama salamu rasmi.
1.1.2 Kauli mbiu itatumika kwenye nyaraka zote zinazohusiana na kikundi.
I.2 NEMBO YA KIKUNDI
I.2.1 Nembo itatumika kwenye nyaraka zote zinazohusiana na kikundi.
I.2.2 Nembo itatumika kwenye sare zote za kikundi.
I.3 ANUANI
I.3.1 Itatumika kwenye barua zote za kikundi.
SEHEMU YA PILI
2.0 UANACHAMA
2.1 SIFA ZA MWANACHAMA
2. 1.1 Mtu yeyote anayeomba kujiunga na kikundi atapaswa kuwa na mdhamini
ndani ya kikundi atakayemsainia kwenye fomu ya kujiunga.
2.1.2 Mtu yeyote anayeomba kujiunga na kikundi atajadiliwa kwanza na
wanakikundi kabla ya kusajiliwa.
2.1.3 Kiambatisho kwenye fomu ya kujiunga na kikundi kitakuwa ni kivuli cha
Kitambulisho cha Taifa(NIDA)/Hati ya Kusafiria , kama nyaraka hizo hazipo
kiambatisho kitakuwa kitambulisho cha mpiga kura ama Leseni ya udereva.
2.1.4 Kila mwanachama atatakiwa kujaza fomu ya kujiunga na kikundi.
2.2 HAKI ZA MWANAKIKUNDI
2.2.1 Mwanakikundi akitaka kujitoa anatakiwa kutoa taarifa mwezi mmoja kabla kwa
maandishi ili aandaliwe stahiki zake.
2.2.2 Mwanakikundi anapaswa kulipa madeni yake yote anayodaiwa na kikundi
kabla ya kujitoa,kama atashindwa kulipa atakatwa kwenye Hisa/Stahiki
zake.
2.2.3 Uhuru wa kutoa maoni uwe na mipaka na maoni yaendane na dhima ya
kikundi.
2.2.4 Mwanakikundi atakuwa na uhuru wa kukopa fedha wakati wowote ikiwa
atatimiza vigezo na masharti ya ukopaji.
2.2.5 Mwanakikundi atabaki na uanachama wake ndani ya kikundi hata
akihama nje ya manispaa kwa kuzingatia sharti la kutokopa zaidi ya hisa
zake.
2.3 WAJIBU WA MWANAKIKUNDI
2.3.1 Kutoshiriki kwenye shughuli za kikundi kama vile magonjwa, misiba,
harusi, miradi n.k, faini yake itakuwa Tsh.5000/=kwa kila shughuli/tukio
ambalo mtu hakushiriki.
2.3.2 Mwanakikundi atakayekiuka maagizo rasmi ya kikundi atatozwa faini ya
Tsh. 5000/=.
2.3.3 Mwanachama atapewa maagizo rasmi ya kikundi mara mbili tu na
asipotekeleza kwa wakati aliopewa atatozwa faini ya Tsh.5000/=.
2.3.4 Mwanakikundi atatakiwa kutoa rambirambi kutokana na Vifo
vinavyotambuliwa na kikundi ambavyo ni mwanakikundi
kufariki,baba,mama,mme,mke au mtoto.
2.3.5 Vikao vya kikundi vitafanyika kila Jumapili ya kwanza ya kila mwezi.
2.3.6 Mwanakikundi ambaye hatatoa ushirirkiano wa kutosha /ipasavyo atapewa
adhabu mojawapo kati ya hizi zifuatazo;
a/ Onyo la mdomo.
b/ Faini ya Tsh.5,000/=.
2.3.7 Kikundi kitakuwa kinagharimia nauli zitakazokuwa zinatumika katika
shughuli za kikundi.
SEHEMU YA TATU
3.0 UONGOZI WA KIKUNDI
3.1 Kiongozi atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake atapewa adhabu
mojawapo kati ya hizi kulingana na kosa alilofanya, adhabu hizo ni;
a. Onyo la mdomo ama la maandishi.
b. Kulipa faini ya Tsh.10,000/=.
c. Fidia
d. Kusimamishwa uongozi kwa muda wa siku tisini (90).
e. Kuondolewa kwenye Uongozi.
3.2 Iwapo kiongozi atajiuzuru, atajitoa ama kutolewa kwenye kikundi ama
akihama uchaguzi wa nafasi yake utafanyika ndani ya mwezi mmoja.
3.3 Iwapo kiongozi atakuwa katika hali ya kuugua kwa muda wa miezi sita (06)
mfululizo nafasi yake itakaimiwa na mwanakikundi atakayependekezwa na
wanakikundi.
3.4 Iwapo kiongozi atafungwa jela nafasi yake itakaimiwa na mwanakikundi
atakayekuwa amependekezwa na wanakikundi hadi uchaguzi utakapofanyika.
3.5 UCHAGUZI WA VIONGOZI
I. Kwa nafasi ya Mwenyekiti na Katibu, yatapendekezwa majina matatu (3)
na kuyapigia kura za siri na mshindi wa kwanza ndiye atakayekuwa
MKUU na anayefuata kwa kura atakuwa MSAIDIZI wake.
II. Kwa nafasi ya Mhasibu, yatapendekezwa majina mawili na kuyapigia kura
za siri atakayepata kura nyingi ndiye atakayekuwa Mhasibu wa kikundi.
SEHEMU YA NNE
4.0 MIKUTANO NA VIKAO VYA KIKUNDI
4.1 UDHURU
a) MSIBA
i. Ruhusa za msiba zitatolewa iwapo mwanakikundi amefiwa na baba,
mama, mke, mume au mtoto.
b) MAGONJWA
i. Ruhusa za magonjwa zitatolewa iwapo mwanakikundi mwenyewe
amelazwa siku ya kikao.
c) KIKAZI
d) SAFARI YA LIKIZO
4.2 Mwanakikundi anawajibika kuwahi vikao na mikutano ya kikundi.
4.3 Mwanakikundi atatakiwa kutoa taarifa ya kuchelewa ama kutofika kwenye
vikao/mikutano ya kikundi saa moja kabla ya kikao/mkutano kuanza.
4.4 Iwapo mwanakikundi atachelewa kutoa taarifa ya kuchelewa kufika kwenye
kikao/mkutano atatozwa faini ya Tsh.1000/=.
4.5 Iwapo mwanakikundi hatatoa taarifa ya kuchelewa kufika kwenye
kikao/mkutano na akachelewa kufika kwenye kikao/mkutano atatozwa faini
ya Tsh.2000/=.
4.6 Iwapo mwanakikundi atachelewa kutoa taarifa ya kutohudhuria kwenye
kikao/mkutano atatozwa faini ya Tsh.3000/=.
4.7 Iwapo mwanakikundi hatatoa taarifa ya kutohudhuria kwenye kikao/mkutano
atatozwa faini ya Tsh.5000/=.
4.8 Iwapo mwanakikundi hatahudhuria kikao/mkutano kwa sababu zisizokubalika
katika Kanuni za Kikundi atatozwa faini ya Tsh.5000/=.
4.9 Iwapo mwanakikundi hatohudhuria kwenye kikao/mkutano atatozwa faini ya
Tsh.5000/=.
4.10 Hata kama kikao/mkutano utaahirishwa kwa sababu ya Akidi kutotimia, faini
iliyotajwa kwenye kifungu cha 4.3,4.4,4.5,4.6,4.7 na 4.8 itabaki pale pale.
4.11 Taarifa zote za kuchelewa ama kutohudhuria kikao/mkutano zitolewe kwa
Mwenyekiti/Katibu wa kikundi kwa njia ya meseji za simu/barua/kufika
mwenyewe kwenye kikao/mkutano.
SEHEMU YA TANO
5.0 MAPATO YA KIKUNDI
5.1 VYANZO VYA MAPATO YA KIKUNDI
5.1.1 ADA YA KIINGILIO
I. Mwanakikundi atasajiliwa kwenye kikundi baada ya kulipa kiingilio cha
Tsh. 50,000/=.
II. Kiingilio kitalipwa mara moja tu wakati wa kujiunga.
5.1.2 ADA YA MWEZI
I. Ada itakuwa inalipwa kila mwezi.
II. Ada ya mwezi ni Tsh. 12,000/=.
III. Kipindi cha Neema (Grace Period) cha kulipa ada kitaanza tarehe 01 hadi
tarehe 07 ya kila mwezi.
IV. Mwanakikundi atakayechelewa kulipa ada ya kila mwezi atapewa kipindi
cha Neema cha siku saba baada ya hapo kama atakuwa hajalipa
atatozwa faini ya Tsh.2000/= ambayo itakuwa ikiongezeka kwa kiasi
hicho hicho kila baada ya siku saba hadi hapo ada itakapokuwa
imetolewa.
V. Risiti itawasilishwa kwenye kikao cha kila mwezi.
VI. Mwanakikundi asipotoa Ada ya kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu (03)
mfululizo bila taarifa rasmi kwa uongozi atakuwa amejifuta uanachama wa
kikundi.
VII. Mwanakikundi atakayelipa ada kwa njia ya simu atalipa makato ya benki.
VIII. Mwanakikundi atahesabika amelipa ada baada ya kuwasilisha risiti ya
malipo.
IX. Mwanakikundi anatakiwa kulipa faini ndani ya miezi mitatu, na ikiingia
mwezi wa nne na kuendelea faini itaongezeka kwa asilimia mia(100%)
kwa kila mwezi.
5.1.3 MICHANGO MINGINE YA KIKUNDI
I. MISIBA
a) Kila mwanakikundi anatakiwa kutoa mchango wa Tsh.5000/= kwa ajili ya
pole kwa mfiwa.
b) Mchango huu utatolewa iwapo mwanachama ataondokewa na baba,
mama, mme, mke au mtoto.
c) Iwapo mwanakikundi amefariki kila mwanachama atatakiwa kutoa
mchango wa Tsh.10,000/=.
d) Mwanakikundi akifariki stahili zake zote atapewa mrithi aliyeainishwa
kwenye fomu ya kujiunga na uanachama.
e) Mwanakikundi ambaye hatakuwa ametoa mchango huu atakatwa
Tsh.5000/= au 10,000/= kutoka kwenye Ada yake ya kila mwezi.
f) Kiasi hicho kilichokatwa kwenye ada yake ya kila mwezi kitatakiwa
kirudishwe ndani ya mwezi mmoja tangu kilipokatwa.
g) Mchango wa rambirambi utatolewa ndani ya siku saba (7) tangu taarifa
ilipotolewa.
h) Mrithi atapewa stahili zake ndani ya siku 14 tangu ilipotolewa taarifa ya
msiba.
II. HARUSI
a) Mchango wa harusi utamhusu mwanakikundi tu.
b) Kila mwanakikundi atatoa Tsh.5000/= ambao utakuwa mchango kwa ajili
ya zawadi .
c) Mwanakikundi ambaye hatakuwa ametoa mchango huu atakatwa
Tsh.5000/= kutoka kwenye Ada yake ya kila mwezi.
d) Kiasi hicho kilichokatwa kwenye ada yake ya kila mwezi kitatakiwa
kirudishwe ndani ya mwezi mmoja tangu kilipokatwa.
e) Taarifa itolewe mwezi mmoja kabla ya harusi.
III. MAGONJWA
a) Kila mwanakikundi atatoa Tsh.5000/= kwa ajili ya mgonjwa.
b) Mwanakikundi ambaye hatakuwa ametoa mchango huu atakatwa Tsh.5000/=
kutoka kwenye Ada yake ya kila mwezi.
c) Kiasi hicho kilichokatwa kwenye ada yake ya kila mwezi kitatakiwa kirudishwe
ndani ya mwezi mmoja tangu kilipokatwa.
d) Mchango utatolewa kwa mwanachama ambaye amelazwa kuanzia siku tatu au
yuko kwenye hali mbaya sana.
e) Mwanakikundi atakayeumwa atapaswa kuleta vielelezo vya matibabu yake ili
achangiwe.
IV. ANAYEHAMA NJE YA MANISPAA
a. Kila mwanakikundi atatoa Tsh.5000/= kwa ajili ya zawadi ya kumuaga
Mwanakikundi anayehama.
b. Mwanakikundi ambaye hatakuwa ametoa mchango huu atakatwa
Tsh.5000/= kutoka kwenye Ada yake ya kila mwezi.
c. Kiasi hicho kilichokatwa kwenye ada yake ya kila mwezi kitatakiwa
kirudishwe ndani ya mwezi mmoja tangu kilipokatwa.
5.2 MIKOPO
5.2.1 Mwanakikundi anayeomba mkopo anatakiwa ajaze fomu ya maombi ya
mkopo.
5.2.2 Mwanakikundi anayetaka kukopa atatakiwa awe na mdhamini mmoja
ndani ya kikundi.
5.2.3 Mwanakikundi atapewa mkopo baada ya kutimiza masharti yote na iwapo
fedha ipo.
5.2.4 Utoaji wa mkopo utazingatia ombi lililotangulia.
5.2.5 Mwanakikundi atatakiwa kurejesha mkopo kwanza kabla ya kukopa tena.
5.2.6 Mwanakikundi mwenye deni lolote la ada,rejesho,faini ama michango
mingine hataruhusiwa kuchukua mkopo.
5.2.7 Mwanakikundi mpya ataruhusiwa kukopa baada ya miezi mitatu tangu
alipojiunga.
5.2.8 Mwanakikundi asiye na ajira ya kudumu ataruhusiwa kukopa kiasi
kinacholingana na hisa yake na kujumlisha kiasi cha nusu ya hisa yake.
5.2.9 Mwanakikundi atakayechukua mkopo atatakiwa kurejesha riba ya 10% ya
mkopo aliochukua.
5.2.10 Iwapo mwanakikundi atafariki akiwa na deni la kikundi na hisa zake ni
ndogo kuliko deni, atasamehewa deni hilo ila hisa zake zitabaki kuwa mali
ya kikundi.
5.2.11 Iwapo mwanakikundi atafariki akiwa na deni la kikundi na hisa zake ni
kubwa kuliko deni, hisa zake zitalipa deni hilo na kitakachobaki atapewa
mrithi wake.
5.2.12 Mwanakikundi atatakiwa kurejesha mkopo kama ifuatavyo;
I. 0000 - 100,000/=Marejesho ya Mkopo na Riba yafanyike ndani ya
mwezi mmoja (01).
II. 100,001-500,000/=Marejesho ya Mkopo na Riba yafanyike ndani ya
miezi mitatu (03).
III. 500,001- 1000,000/= Marejesho ya Mkopo na Riba yafanyike kila
mwezi ndani ya miezi sita (06) kwa uwiano wa moja ya sita (1/6).
IV. 1000,001- 1200,000/= Marejesho ya Mkopo na Riba yafanyike kila
mwezi ndani ya miezi saba (07) kwa uwiano wa moja ya saba(1/7).
V. 1200,001-1500,000/= Marejesho ya Mkopo na Riba yafanyike kila
mwezi ndani ya miezi nane (08) kwa uwiano wa moja ya nane(1/8).
5.2.13 Kama mwanakikundi atachelewa kurejesha rejesho lake la kila mwezi
atapewa kipindi cha Neema cha siku saba ,akiingia siku ya nane na
kuendelea rejesho lake litapigiwa 10% kama faini.
5.2.14 Iwapo mwanakikundi ameshindwa kurejesha mkopo wake kwa wakati na
kwa masharti aliyopewa sheria za kikundi na za nchi zitafuatwa
5.2.15 Mtu yeyote asiyekuwa mwanachama hataruhusiwa kupewa mkopo.
5.2.16 Mhasibu atatakiwa kuitaarifu Kamati ya Fedha na Mikopo kabla ya
kupitisha fomu ya mkopo wa mwanakikundi.
5.2.17 Watia saini watapewa nauli na kikundi watakapokuwa wanashughulikia
masuala ya fedha benki.
5.3 MADENI YA KIKUNDI.
I. Kila mwanakikundi anahusika kikamilifu na madeni ya kikundi kama
deni hilo halikusababishwa na uzembe wa mwanakikundi.
II. Deni binafsi la mwanakikundi si deni la kikundi na kikundi hakitahusika
kwa vyovyote vile.
III. Mkopo utakaohusu kikundi, wanakikundi wote washirikishwe katika
hatua zote na muhtasari uwepo wa kuthibitisha maazimio ya uchukuaji
wa mkopo huo.
SEHEMU YA SITA
6.0 UTUNZAJI WA MALI NA FEDHA ZA KIKUNDI
6.1 UTUNZAJI WA FEDHA ZA KIKUNDI.
I. Kila mwanakikundi ataweka Ada, Marejesho na Faini yake kwenye
Akaunti ya kikundi.
II. Mabadiliko yoyote ya Akaunti ya Benki ya kikundi yatatakiwa
kuwasilishwa, kujadiliwa na kupitishwa katika vikao vya kikundi.
III. Mhasibu na Kamati ya Fedha na Mikopo wataandaa Taarifa ya Fedha
ya Nusu mwaka na ya mwaka na kuiwasilisha kwa kamati Tendaji ya
kikundi.
6.2 KIKOKOTOO CHA HISA, kitakuwa;
JUMLA YA ADA ALIZOLIPA MWANACHAMA TANGU ALIPOJIUNGA NA
KIKUNDI JUMLISHA JUMLA YA FAIDA ILIYOPATIKANA KILA MWEZI KWA
MIEZI YOTE TANGU ALIPOJIUNGA NA KIKUNDI HADI TAREHE YA KUJITOA
/KUTOLEWA KWENYE KIKUNDI GAWANYA KWA IDADI YA WANACHAMA
KWA KILA MWEZI.
SAWA NA;
JUMLA YA ADA + JUMLAYA FAIDA YA KILA MWEZI KWA MIEZI YOTE
IDADI YA WANACHAMA KILA MWEZI
SEHEMU YA SABA
7 .0 KUVUNJIKA KWA KIKUNDI
I. Kikundi kitavunjika iwapo robo tatu ya wanakikundi wameridhia kuvujika.
II. Endapo kikundi kitabaki na wanakikundi wawili, kitatakiwa kivunjwe.
III. Kikundi kikivujwa/kuvunjika wanakikundi ambao watakuwa hai ndio watakao
gawana mali zote za kikundi.
IV. Maamuzi ya kuvunja kikundi yatafanyika katika kikao halali cha kikundi na
muhtasari utaandikwa.
V. Kabla ya kuvunja kikundi, pesa zote za kikundi zitatakiwa kuwekwa kwenye
Akaunti ya kikundi.
VI. Kabla ya kuvunja kikundi, madeni yote ya kikundi yanatakiwa kulipwa kwanza.
VII. Kabla ya kuvunja kikundi, mali zote za kikundi zitatakiwa kuwasilishwa
kwenye kikao cha kuvunja kikundi.
IKICHA…,
TUINUANE KATIKA MAENDELEO
No comments:
Post a Comment